Mambo ya Dada Njoo Darajani hayo yakiwa yameshamiri kwa bidhaa mbalimbali zikiwa zimewekwa katika henga kuvutia wateja na wapita nijia katika eneo hilo lilioko mkabala na Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni ikiwa ukuta wa skuli hiyo ndio henga ya bidhaa hizo.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Kisiwandui wakiwa katika maeneo ya michezani wakirudi majumbani baada ya kumaliza vipindi vya masomo kwa siku hiyo. mdau wewe unakumbuka ulivyokuwa na umri huu ulikuwa na mchezo mwingi na kuchelewa kurudi nyumbani kwa mchezo wa njia na wanafunzi wezako kama wilovyo wanafunzi hawa wakiwa katika mchezo wakati wakirudi majumbani. 
Mfanyakazi wa Baraza la Manispa Zanzibar akitunza usafi wa mazingira ya marikiti ya mbogamboga, ili kuweka eneo hilo safi, kwa wananchi wanaofika katika soko hilo kukuta mazingira ya usafi wanapofata bidhaa katika soko hilo.
No comments:
Post a Comment