Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto)akimkabidhi Bendera Nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Canavarro, akishuhudia Makamu Mwenyekiti wa ZFATaifa Alhaj Haji Ameir.makabidhiano hayo yamefanyika katika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) wakati wa kuikabidhi bendera na kuiaga katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. ili kuipeperusha katika Michuano wa Kombe la Chalenji Nchini Uganda,
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Bausi akizungumzia uimara ya timu yake ilivyojiandaa katika michuano hiyo ya Chalenji ilipokuwa ikiaga na Waziri wa Michezo Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya bwawani. Zanzibar .
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes Nadir Haroub Canavarro akitoa shukurani kwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na kuahidi kuipeperusha Vyema Bendera ya Zanzibar katika Michuano ya Chalenji itakayofanyika Uganda.
No comments:
Post a Comment