Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Wazazi, Kamati na Kituo cha Kulelea Watototcha SOS hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AIi Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wazazi, Kamati na Kituo cha kulelea watoto wa SOS uliofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Uongozi wa wazazi, Kamati na Kituo cha kulelewa watoto cha SOS hapo ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Na Othman Khamis Ame
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Uongozi wa Wazee, Kamati pamoja na Kituo cha Kulelea Watoto cha SOS Kiliopo Mtaa wa Mombasa nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kituo hicho Nd. Suleiman Mahmoud Jabir alisema katika kutunisha mfuko wa kuhudumia Kituo hicho uongozi huo umeamuwa kuanzisha utaratibu maalum wa michango kwa lengo la kuondosha utegemezi ambao unaonekana kupunguwa kutoka kwa wafadhili.
Ndugu Suleiman alisema msaada wa wahisani kuendelea kuhudumia Kituo hicho umepunguwa wakati kituo hicho hivi sasa kinakabiliwa na tatizo la miundo mbinu ya maji machafu, pamoja na kuchakaa kwa madarasa ya Skuli hya Kituo hicho.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Michango ya kutunisha mfuko wa Kituo hicho Dr. Mohd Hafidh alisema Uongozi huo umeamua kujipanga katika mazingira ya kuanza kujitegemea wenyewe .
Dr. Mohd Hafidh alisema utaratibu wa kuanzisha Clabu ya kujitolea pamoja na shughuli maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mfuko huo umelenga kukabiliana na ongezeko la wahitaji wakati hali ya uchumi kidunia imezorota.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarBalozi Seif Ali Iddi alisema kutokana na umuhimu na ugumu wa kazi ya ulezi Kituo hicho kinapaswa kusaidiwa Kitaifa kwa vile nguvu za wahisani wa kimataifa zimeanza kupungua.
Balozi Seif alifahamisha kwamba ubunifu wa miradi kwa hivi sasa ni jambo la msingi katika azma ya kukiendeleza vyema Kituo hicho ambacho kiko katika changamoto ya ongezeko la wanafunzi kutokana na ubora wa elimu inayotolewa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameahidi kujiunga katika klabu ya kujitolea ya Kituo hicho pamoja na kushiriki katika shughuli yao maalum ya mchango ili kushajiisha umma kuunga mkono suala hilo muhimu kwa hatma njema ya watoto wa Kituo hicho.




No comments:
Post a Comment