Maelezo Zanzibar 2/12/2012
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzia Dkt Mohammed Gharib Bilal amehudhuria kuapishwa kwa Rais wa Mexico ENRIQUE hapo jana mjini Mexico
Kwa mujibu wa taarifa iliyotufikia ofisini kwetu kupitia ofisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington Amerika Suleiman seif amesema kuwa sherehe hiyo ya kuapishwa ilikuwa ya aina yake na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
Amesema kuwa Jumla ya Marais wa nchi 36 wamehudhuria katika sherehe hiyo.
Mbali na Marais wa nchi hizo pia Makamo wa rais wa nchi zipatazo 18 wameshiriki katika kuapishwa Rais huyo wa Mexico.
Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt Bilal amehudhuria sherehe hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Mexico ENRIQUE amefurahishwa sana na Tanzania kwa ujio wa Makamo wa Kwanza wa Rais Dkt Bilal katika sherehe hiyo kwa kumuwakilisha Rais wa Tanzania.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 2/12/2012
No comments:
Post a Comment