Habari za Punde

Sakata la kugawana fedha Zanzibar Heroes - Wachezaji wana haki ya kusikilizwa

Na Ali Sultan
 
ZFA – naomba muelewe kuwa hakuna mgogorro usiokuwa na sulhu – every crisis is resolvable, hiyo ndio msingi mkuu wa utatuzi wa migogoro duniani: understanding differences, acting on commonalities.

Iwe ni mgogoro mdogo tu kama huu wa ZFA na wachezaji, kimsingi tunauuita ‘hitilafu tu za kiutwala’ au mgogoro uwe mkubwa wenye kunasibisha mamlaka ya nchi kwa nchi.

Kwa mfano, mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania; au tuseme hata mgogoro unaohusu maslahi ya kisiasa, utawala na uongozi – kwa mfano viongozi wakuu wa nchi ya Madagascar.

Angalia, Tanzania inajaribu sana kusuluhisha mgogoro huu wa mpaka kati ya Malawi-TZ kwa njia ya sulhu, na wanajaribu sana kuepuka vita au sulhu ya mfumo wa mahkama.



Bernard Membe, foreign secretary is doing his best n HE President Kikwete is charting his diplomatic and negotiating skills kumaliza switilfahamu hii kimazungumzo na kimaelewano zaidi juu ya meza ya mazungumzo (dialogue, face to face, na kuandaa mediation team n.k).

Kadhalika President Kikwete ameipandisha chati sana TZ na yeye mwenyewe katika kutafuta sulhu ya ‘mtafaruk wa kisiasa’ wa nchi ya Madagascar. Dunia ya sasa, imejaa mizozo, lakini utatuzi wake upo.

Itakuwa ni mushkeli mkubwa sana kama ZFA, na kama viongozi, mtashindwa kusuluhisha mgogoro huu wa ndani zaidi, ambao gharama yake ni kubwa kuliko dola 500.

Kuijenga timu ya taifa mpya ni gharama ya mabilioni kuliko hizo dola 10,000.

Naomba ZFA muige mifano kama hiyo. Uamuzi mliotoa wa ‘kufunga milango yote, na madirisha yote’ katika suala la kuleta sulhu baina yenu na wachezaji linatia aibu sana.

Ina maana mnanataka kusema kuwa ‘there’s no room for negotiation’? Mmeona wapi hilo? Mkiwa hivyo, ni dalili za utawala wa kibabe au kibri n jeuri ya kiutawala (arrogance of power).

Iwe vyovyote vile,uamuzi wenu ZFA dhidi ya wachezaji hauko sahihi, na ninaomba mzipitie tena sheria zenu zenyewe za ZFA, pamoja muangalie vizuri sana sera ya michezo ya Zanzibar. Hapa mnauwa michezo, na sio kuendeleza michezo.

Naomba mnifahamu vizuri kuwa sina nia ya kutetea wachezaji, ila hukumu iliyotolewa ni kubwa kuliko kosa lenyewe.

Unapotoa/kufanya justice, siku zote kisheria, unatakiwa justice has to be seen, ionekane, watu waione kama kweli imefanyika justice, iwe fair, reasonable (hapa naomba msome kanuni n sheria za FIFA) mtapata kujua nini ninasema.

FIFA wao katika kufanya hili ‘fair justice’ au justice to be seen by others – ndio maana wameweka mfumo wa ‘reply’kujua kama kweli goli lililofungwa ni halali, au la, na kama referee amependelea– kadhlika wachezaji nani amemfanyia foul mwenzake, na kama mwamuzi hakuona –ndio hizo reply zinachezeshwa mra moja, mbili, tatu n.k n.k. Pamoj na hayo, wanakuwepo observers wengine ili kuhkikisha haki, na sheria imefanyika.

Pamoja na yote hayo, ZFA, mmeona wapi hukumu iliyokuwa hain rufaa/appeal.

Yaani viongozi ZFA wakiamua ndio wameamua – hakuna kutaka rufaa. Again, hizi ni khulka za kibabe, lazima mtoe ‘room’for appeal, na waliodhulumiwa au waliodhuriwa wasikilizwe kama haki ya msingi ya mkosa na mkoswa.

Hivi tuseme leo serikali iamue kwa mkusudi kufanya upekuzi wa utendaji wenu hpo, matumizi, na manunuzi, kweli mtakuwa “wasafi”?

Na je, mchukuliwe hatua za kisheria. Mshukuru kuwa serikali zetu mbili ni wastahamilivu sana (tolerable) san asana. Inavumilia mambo mengi, mengine si ya kuvumilika. Lakini patience yake kwa wananchi wake ndio imezaa hisia z upendo, uvumilivu, amani na utulivu.

ZFA na uongozi wake lazima muonyeshe ability of leadership, one is tolerance+ patience.
Na kama hamna hizi skills, quality of leadership – siku hizi wapo watu wanatoa mafunzo kama haya (coaching), zitakusaidieni sana.

ZFA mjue kuwa image yenu sio nzuri kwa umma wa Zanzibar, kwa siku nyingi sasa. Lazima mjirekebishe sana.

Napenda kuipongeza timu hii ya taifa kwa juhudi na bidii waliofanya mpaka kufikia hapo mshindi wa tatu.

Wengi tuliamini timu yetu hii inaingia fainali na kuleta kombe nyumbani. Pongezi pia kwa kocha Buasi (Roger Miller) – yeye alikuwa hatulii kabisa uwanjani kama vile enzi za Michael Platin au Jurgen Kilinsmann.

Mwisho, napenda kuto wito kwa serikali iangalie upya adhabu hii ya kibabe na itoe amnesty kwa wachezaji hawa. Lakini tujue kuwa lesson learnt hapa ni kuwa masindano yanayofuata ijulikane mapema pesa ni za nani, analipwa nani, na zisiwe katika mfumo wa cash/iwe cheque.

Wachezaji wanayo HAKI ya Kusikilizwa.

1 comment:

  1. good article

    tabu yote hii imekuja kwa sababu ya dola mia tano mia tano tuu.

    ikiwa hii zawadi ni cash yaani ilikusudiwa wachezaji. ingekuwa inatakiwa kupewa nchi basi isengekuwa dola 10k

    ZFA wamekosa ustahmilivu - ni walafi basi

    wachezaji wakizipeleka hizi pesa ZFA hawatopata kitu.

    msimamo huo huo.




    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.