Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA wa soka barani Afrika timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo), wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo wakiwa na msafara wa watu 32.
Timu hiyo itatua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mnamo saa 11:00jioni kwa ndege ya Precision Air ikitokea Lusaka.
Miongoni mwa watu hao, kuna wachezaji 24,ambao wanakuja nchini kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stara, ikiwa chini ya kocha Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji wanakuja na kikosi hicho ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Mabingwa hao wa Afrika wanatarajiwa kushuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi Disemba 22, mwaka huu, mchezo utakaoanza saa kumi kamili jioni.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Disemba 12 mwaka huu chini ya kocha Kim Poulsen kujiandaa kwa ajili ya pambano hilo.
No comments:
Post a Comment