INALILAH WAINA ILAIH RAJHUN.
Msanii wa Kikundi cha Taarab cha East Afrika Melody,na Mtunzi wa Nyimbo katika kikundi hicho, Lamania Shaban, amefariki leo asubuhi nyumbani kwake Mbagala mjini Dar-es- Salaam. na mipango ya mazishi inafanyika na anategemewa kuzikwa kesho saa kumi jioni.
Marehemu alikuwa muazilishi wa Bendi ya Melody iliyokuwa na makazi yake Mlandege Zanzibar na kuwa na cheo ya Mkurugenzi wa Muziki katika kikundi hicho hadi mauti yanamkuta.
Marehemu alikuwa akishumbulia na maradhi ya baridi kwa muda wa miaka mitatu sasa hadi mauti yanakuta leo alfajiri nyumbani kwake mbagala.Mungu amlaze pema peponi Amin.
No comments:
Post a Comment