Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kuelekea nchini India kwa ajili ya ukaguzi wa afya.
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa kiongozi huyo kwenda nchini India kwa ajili ya ukaguzi wa afya kila baada ya miezi sita, tangu alipofanyiwa operesheni ndogo ya magoti mwaka 2011.
Maalim Seif anatajiwa kurejea nchini mwanzoni mwa mwezi ujao.
Jambo hili si la upotevu wa fedha za Serikali? au mnajua kumlaumu Makamu wa Pili wa Rais kuwa anapoteza pesa za serikali kwa kusafiri, Makamo wa kwanza anajilipia mwenyewe gharama hizi? amkeni nyie mlioamshwa na uamsho.
ReplyDeleteWacha wivu ivi utafurahia kesho au mtondogoo tupate kiongozi anatembea kama DOSTI, kwa nini asiende kuangaliwa afya yake kwa vile wamemshauri madaktari arudi huko huko ?
DeleteHugo Chávez Rais wa Veneziwela Amerika ya Kusini Mara nyingi hutibiwa Cuba na haliyakuwa nchi yeke kuna watalamu mahiri kuliko Zanzibar.
ReplyDeleteKwa hio na kiongozi Kama Maalim Seif Kutibiwa India sio mbaya kwani ni safe kwa usalama wake, maara ngapi Maalim Seif walimkosa kumuuwa kwa Sumu?.
Mtu kama Maalim Seif ana wabaya wengi Ndugu zake mwenyewe viongozi wa Smz na walijaribu mara nyingi kumtilia Sumu lakini tu zake zikaliko.
Sasa kutibiwa nje ya nchi ni bora zaidi kuliko hapa mtu kama yeye, simunajuwa uharamia wa viongozi wa Tanganyika kuwa-remote Smz.
mimi sina wivu na kiongozi yoyote , ila wenzetu mnaangali aupande mmoja tu, sote tunataka viongozi wenye afya nzuri na wawe na nguvu ya kufanya kazi , isipokuwa mnashusha lawama kwa viongozi wa uoande fuani wanapokwenda matibabubi au ziara ya kikazi, ndio nimeona tuchangiane mawazo ili tuelewane kama tulivukubaliana kuwa wamoja
ReplyDeleteTAHADHARI MATUMIZI YA KUGHA:
ReplyDelete1) CHOYO; ni uchungu au hasira anayoipata mtu pale anapoona mwengine amepata au kufaidika na kitu au huduma fulani.
2)WIVU; ni uchungu au hasira anayoipata mtu pale anapoona mwingine anafaidika au kutaka kufaidika kimapenzi na Mke, Mume au Mpenzi wa mtu huyo.
Nadhani ingekua sahihi kwa wadau waliotoa maoni hapo juu kutumia neno 'CHOYO' kulingana na muktadha wa mada husika.
CCM hawashindwi kitu kwani wakitaka kumfanyia Malim Seif wanaweza kumfanyia hata huko India kwani hamkumbuki kuna viongozi wetu wazuri ambao wameuliwa uk? huyo maalim seif ni mwenzao bwana kwa walio na akili timamu hili wanalijuwa kama mwenzao CCM!! Kama angekuwa sio mwenzao washammaliza zamani!!.
ReplyDelete