Othman Khamis Ame(OMPR)
Ujenzi wa Vituo vya Afya unaoendelea kufanywa na walio wengi katika maeneo mbali mbali nchini umesaidi kutoa faraja na mchango mkubwa kwa serikali katika dhana nzima ya kuenezwa kwa huduma za afya ndani ya jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sewif Ali Iddi alisema hayo mara baada ya kuweja jiwe la msingi la nyongeza ya jengo la Kituo cha afya Sebleni kiliopo ndani ya Nyumba za wazee Sebleni Wilaya ya Mjini.
Balozi Seif alisema kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu liliopo hapa Nchini vituo vidogo vya afya kwa kiasi fulani vinatoa mchango mkubwa unaosaidia kupunguza msongamano wa upatikanaji wa huduma za afya katika Hospitali kubwa ambazo badi ni kidogo Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiagiza Wizara ya afya kujitahidi kuwaandaa Madaktari sambamba na wauguzi watakaokidhi mahitaji ya vituo vinavyoanzishwa na wananchi katika maeneo tofauti.
Aliwapongeza wananachi wa majimbo yanayokizunguuka Kituo hicho kwa kupata huduma pamoja na
Aliwapongeza wananachi wa majimbo yanayokizunguuka Kituo hicho kwa kupata huduma pamoja na
Viongozi wao kwa uamuzi wao wa kuongeza jengo zaidi katika kituo hicho.
“ Nimefarajika kuona mchango wa shilingi mia mbili mia mbili uliokuwa akitolewa na wananachi wakati wakipatiwa huduma kwenye kituo hicho umekuwa chachu ya kujengwa jengo hilo la Pili katika Kituo hicho. Sina budi kumpongeza mama aliyesimamia kazi hiyo ngumu kama ingekuwa tumepewa sisi akina baba tungekuwa tushazilia tasi”. Alisisitiza Balozi Seif.

Aliitahadharisha Jamii kuzingatia zaidi uzazi wa mpango utaokwenda sambamba na ukuaji wa uchumi wa Taifa ili kuwa na kizazi kitachoweza kuhudumiwa vyema.
Balozi Seif alifahamisha kwamba watoto wanawajibika kupatiwa huduma za afya pamoja na haki ya elimu mambo ambayo yamesisitiza na kuelekezwa katika mvitambu na maamrisho ya Dini.
Katika Kuunga mkono juhudi za Wananachi hao wa majimbo yanayokizunguuka kituo hicho cha afya cha Sebleni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameahidi kusaidia utiaji wa silingi jengo lote la Kituo hicho.
Akimkaribisha Balozi Seif Waziri wa Afya Mh. Juma Duni Haji aliwaahidi Wananachi hao kwamba Wizara hiyo italikabidhi jengo lililokuwa ghala wakati wa ujenzi wa Jengo la kituo cha damu salama damu kwa wananchi hao ili lifanyiwe matengenezo kwa ajili ya huduma za Akina mama.
Waziri Juma Duni alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na Kituo hicho kupandishwa daraja la pili kutokana na juhudi za wananchi na watendaji wa Kituo hicho.
Mapema Daktari dhamana wa kanda ya unguja Dr.Fdhil Mohd alieleza kwamba Wizara ya Afya imejipanga kuanzisha huduma maalum za afya ndani ya jamii kwa lengo la kuzuia maradhi badala ya kusubiri kutibu.
Dr. Fadhil alisema mpango huo utashuka zaidi kwa jamii katika kuongeza nguvu za kinga zitakachochangia kupunguza mzigo kwa hospitali kubwa ambazo hivi sasa zimekuwa na msongamano wa wagonjwa.
Katika risala yao iliyosomwa na Bibi Mwatima Abdulla Haji Wananachi hao wameelezea changa moto zinazowakabili katika ukamilishaji wa Kituo hicho cha nyongeza cha afya sebleni.
Katika risala yao iliyosomwa na Bibi Mwatima Abdulla Haji Wananachi hao wameelezea changa moto zinazowakabili katika ukamilishaji wa Kituo hicho cha nyongeza cha afya sebleni.
Walizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na Vyoo,mafeni, masinki pamoja na mahardboad.
No comments:
Post a Comment