Viongozi na Wachezaji wa timu ya Mji Mkongwe wakifuatilia mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la CCM kutimia miaka 36, iliozishirikisha timu tano za Wilaya ya Mjini Kikwajuni, Rahaleo Kwahani, Jangomba na Mji Mkongwe, zinazofanyika katika uwanja wa Mao.timu ya MjiMkongwe imeshinda 1-- 0
Beki wa timu ya Jimbo la Kikwajuni Hassan Omar, akimkata mchezaji wa timu ya Jimbo la Mjimkongwe, wakati wa mchezo wa kuwania Kombev la CCM Wilaya ya Mjini, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Mao, timu ya MjiMkongwe imeshinda 1--0
Mashabiki wa Jimbo la Kikwajuni na Mji Mkongwe wakitambiana wakati wa mchezo wao uliofanyika katika uwanja wa Mao timu ya Mji Mkongwe imeshinda 1--0.
Mbunge wa Jimbo la Rahaleo na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Abdalla Juma Mabodi akitowa huduma ya kwanza kwa mchezaji wa timu ya Mji Mkongwe kuumia goti kutokana na kugongana namchezaji mwezake wakati wakiokoa mpira golini kwake.
Mbunge wa Rahaleo Dk. Abdalla Juma Mabodi akisaidiana na viongozi wa timu ya MjiMkongwe kumbeba mchezaji huo baada ya kuumia katika mchezo huo na kukimbizwa kupata huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu zaidi.
Viongozi wa timu ya Kikwajuni wakifuatilia mchezo huo ambao wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0 na timu ya Jimbo la Mji Mkongwe
No comments:
Post a Comment