Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) Amwaga Vifaa Bububu



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Bububu wakati wa sherehe wa kukabidhin Vifaa kwa wananchi wa jimbo hilo vilivyotolewa na Mwakilishi Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) ikiwa ni kutimiza ahadi alioitowa wakati wa Uchanguzi Mdogo uliofanyika mwaka jana.

Wananchi wa Jimbo la Bububu wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia katika viwanja vya Kwageji Kijichi Bububu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi Kiongozi wa timu mpira za Jimbo hilo, kwa niaba ya timu za Jimbo hilo jumla ya timu za mpira za daraja la Pili, Tatu na Central zimekabidhiwa Seti ya Jezi Stoking Viatu vya mpira na mipira miwili, ilimkushiriki vizuri katika michuano inayoshiriki, vifaa hivyo vimetolewa na Mwakilishi BHAA, ikiwa ni ahadi alioitowa wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mdogo uliofanyika mwaka jana.

Mwakilishin wa Jimbo la Bububu Hussein Ibrahim Makungu (BHAA)akimkabidhi ufungo wa Vespa Makamu wa Pili  Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ili kutoa kwa Viongozi wa Matawi ya CCM matano ya Jimbo hilo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimkabidhi mmoja wa Watoto wenye ulemavu walioko katika jimbo hilo Wheel chair ili kutowa huduma zao za kila siku jumla ya wheelchair kumi zimetolewa kwa ajili ya Watu wenye ulemavu. kulia Mwakilishi wa jimbo hilo Hussein Ibarahi Makungu (BHAA) akimsalimia  mtoto huyu.

Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi fungo za gari la Wanafunzi lililotolewa na Mwakilishi wao kwa ajili ya kutoa huduma ya usafiri wakati wa kwendea skuli na kurudi majumbani wakati wa mchana na jioni.

Wananchi wa Jimbo la Bububu wakishuhudia kukabidhiwa Vifaa mbalimbali kwa ajili ya Jimbo hilo.

Wachezaji wa timu za mpira zilioko katika jimbo hilo wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Vifaa vya michezo kwa ajili ya timu za Jimbo la Bububu vikiwa katika uwanja wa mpira kwa Geji  Seti za Jezi, Viatu na Mipira.

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Hussein Ibarahim Makungu (BHAA), akiwa na viongozi wa jimbo la Bububu wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, katika viwanja vya mpira vya Kwageji Kijichi Bububu.
Gari za kuzolea takataka katika jimbo la bububu zilizotolewa na Mwakilishi wao, ikiwa ni ahadiyake alioitowa wakati wa kampeni yake katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka jana.
Vespa kwa ajili ya kazi za Matawi ya Jimbo hilo lina matawi matano.
Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Hussein Ibarahim Makungu (BHAA) akizungumza na Wananchi wa jimbo lake baada ya kukabhidhiwa Vifaa mbalimbali kwa ajili ya Jimbo hilo ikiwa ni kutimiza ahadi alioitowa mwakilishi huyu wakati wa Uchanguzi mdogo wa jimbo hilo kufuatia kwa kifo cha Mwakilishi wa jimbo hilo Salum Amour Mtondoo, kilichotokea mwaka jana.
Mipira ya Maji na Matanki yake kwa ajili ya kutowa huduma ya maji safi na salama kwa Wananchi wa jimbo hilo.

Viti vya Wheelchair, kwa ajili ya Watu Wenye Ulemavu vimetolewa na Mwakilishi kwa ajili ya Wananchi wa jimbo hilo wenye ulemavu.
TV zimetolewa na Mwakilishi kwa ajili ya Matawi Matano ya Jimbo hilo.
Baskeli kwa ajili ya watoto. 
Basi la Wanafunzi wa Jimbo la Bububu.






2 comments:

  1. ndio nini?? msokuwa na haya nyie...lakini mungu atakulipeni inshalah kwa kusababisha kifo cha mtoto wetu wa miaka 14

    ReplyDelete
  2. Katoa yeye Muwakilishi au kawakilisha chama? Maana vitu vyeney thamnai nyingi sana au mie ndio sijui Muwakilishi huyo ana fulusi kiasi gani?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.