Habari za Punde

NCCR - Mageuzi , TAde watoa maoni kwa tume ya mabadiliko ya Katiba

 Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na uongozi wa NCCR-Mageuzi uliofika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.
 Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Ndg. James Mbatia akiongea katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati chama chake kilipokwenda katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba na katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid.
 Baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wakifuatilia mkutano kati ya chama chao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013) wakati chama hicho kilipowasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya.
 Rais wa Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA) Ndg. John Chipaka akimkabidhi Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ndg. Mwatumu Malale maoni ya chama chake kuhusu katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013).

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ndg. Mwatumu Malale akiongea na uongozi wa Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA) chini ya Rais wake Ndg. John Chipaka wakati chama hicho kiliwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013).
 
Picha na Tume ya Katiba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.