Na Pascal Michael, Musoma
SERIKALI imetakiwa kuvidhibiti vyombo vya habari vinavyokashifu na kukejeli dini au madhehebi ya watu wengine.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu wa jimbo Katoliki Musoma, Mhashamu Michael Msonganzila katika sherehe za Maria Mtakatifu Mama wa Mungu zilizofanyika katika Kanisa Kuu Musoma na kuhudhuriwa na mamia ya waumini.
Alisema baadhi ya redio za dini zimekuwa zikitumia vipindi virefu kukashifu dini au madhehebi mengine, hivyo tabia hiyo inapaswa kudhibitiwa hara iwezekanavyo.
Alisema vyombo vya habari hususan vya dini vimesajiliwa kwa ajili kuwafundisha waumini wake maadili mema na jinsi ya kumcha Mungu lakini badala yake vimegeuzwa kushambulia madhehebi na dini nyegine.
Askofu huyo aliitanabahisha serikali kwamba ni vyema ikachukua hatau za haraka kuvidhibiti vyombo hivyo ili visiwe chanzo cha uchochezi wa kidini.
“Tabia na mienendo ya kukashifiana ikomeshwe na kuwa kitu kimoja, vyombo vya ulinzi na usalama vichukue hatua za haraka,” alisema.
“Tukianza kukashifiana tutafika wapi, amani sio vita jamani pasipokuwa na amani maendeleo hayawezi kupatikana, ” alisema.
Katika hatua nyingine, Askofu Msongazila aliwataka wale wote wanaomkashifu Baba wa Taifa waende kwenye kaburi lake kijijini Butiama na wayasema maneno hayo ili Mwalimu aweze kuwaombea kwa Mungu awasamehe dhambi hiyo.
Alisema kumekuwa na upotoshwaji mkubwa juu ya maisha ya Mwalimu Nyerere jambo ambalo ni hatari kwa kizazi kijacho ambacho hakikubahatika kumuona kiongozi huyo enzi za uhai wake.
Alisema upotoshaji huo usipodhibitiwa utapotosha historia ya Tanzania hasa juu ya mtu ambeye ametengezeza historia nzuri ya taifa .
Aliwataka Wakiristo kote nchini kusali na kuiombea amani ya Tanzania idumu.
Aidha alitoa mapendekezo kwa taasisi na mamlaka zinazosimamia matangazo na vyombo vya habari kuhakikisha vyombo vya dini vinatumika kueneza imani kwa waumini na amani na siyo kukashifu watu na imani
Kwa tafsiri pana, vyombo vya khabari ni pamoja na mitandao ya kijamii.
ReplyDeleteHivyo basi, kwa kutekeleza ombi hili la maaskofu serikali ingeanza na mtandao wa JAMII FORUM!