Na Gilbert Massawe
WATOTO tisa wamezaliwa katika mkesha wa kuuaga mwaka 2012 katika hospitali ya wazazi Mwembeladu mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa daktari muuguzi wa hospitali hiyo, kati ya watoto hao saba walikuwa wanaume na wawili wanawake.
Daktari huyo alisema watoto wote walizaliwa wakiwa hai na afya njema.
Watoto wawili walizaliwa kuanzia usiku wa kuamkia jana na wengine saba walizaliwa alfajiri ya Januari 1, 2013.
Aidha alisema, watoto hao walizaliwa kwa njia ya kawaida na mama zao wanaendelea vizuri huku wengine wakiwa wamesharuhusiwa kurejea nyumbani.
No comments:
Post a Comment