Habari za Punde

Vuai :CCM acheni kusemana

Na Madina Issa
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuacha kutumia muda mrefu kwa kusemana na kutetana, badala yake watumie muda huo kuimarisha chama ili kipate ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Maneno hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Vuai Ali Vuai kwa nyakati tofauti wakati akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mjini katika ukumbi wa CCM Mkoa huko Amani jana.

Aliwataka viongozi wa CCM wavumiliane na wasameheane kutokana na kasoro ndogo zilizotokea baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa chama hicho.

Alisema makosa ambayo hayawezi kuvumilika katika Chama ni yale yanayotokana na itikadi, sera, miongozo na maamuzi ya chama yaliyoamuliwa na vikao halali.

Alisema mwanachama na hasa kiongozi atakaekwenda kinyume na sera na itikadi ya CCM hatavumiliwa.

Aliwataka wanaCCM kuyavunja mara moja makundi yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa chama na jumuiya zake.

Alisema wanachama waliobahatika kupata kura za kutosha na kupata nafasi za uongozi katika chama hawanabudi kushirikiana na wale wanachama wenzao amabo hawakubahatika kuchaguliwa.

Nao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wa Mikoa hiyo wameahidi kuwapa ushirikianao wajumbe wapya wa sekreterieti ya kamati maalum ya NEC Zanzibar.

2 comments:

  1. No point of sending message while you restrict WHAT FOR while one can get the same from wavuti you are just selfish, remember freedom of speech which you workj for, don't be selfish

    ReplyDelete
  2. Every blogger is fully responsible with his blog as well as its contents. Moreover, this blog has its theme and that is the vision of the blog owner. So if a reader sees things in a different way, the best move is to engage the blogger in a very respectful way in order to continuous improve this blog. But at the end of the day we need to respect the blogger and his theme. Let us not force him to do what we want.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.