Radhia Abdalla, Pemba
Mkurugenzi Idara ya Habari,Maelezo Zanzibar Yusuf Omar Chunda amewataka waandishi wa Habari Nchini kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao wakiwa na leseni za uwandishi wa habari (PRESCARD) ili kuhakikisha kwamba wanafanya kazi zao hizo kwa mujibu wa sheria No5 ya mwaka 1988 ya magazeti .
Hayo ameyaeleza leo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali huko katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Chake chake Pemba juu ya utendaji wa kazi za Idara hiyo kwa mwaka 2012 na kuomba mawazo yao kwa utendaji wa kazi kwa mwaka 2013.
Amesema kuwa na kitambulisho kitamrahisishia mwandishi huyo kufanya kazi kwa mujibu wa sheri na kupata habari anazozihitaji kwa wahusika bila ya matatizo ambazo zitaweza kuchapishwa na kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mkurugenzi huyo amewataka waandishi hao kutopuuza agizo hilo la kuwa na kitambulisho kwani ni kwa faida yao wenyewe kutokana na kazi zao wanazozifanya kila siku.
Chunda amesema kuwa viongozi wasionekane wagumu pale wanapotaka kutoa habari kwanza kwa kuuliza waandishi vitambulisho vyao kwani wao wanahitaji uhakika wa
mwandishi huyo kama amepata kibali cha kuandika habari nchini kama sheria inavyotaka .
Amesema kuwa ni vyema kwa waandishi kuelewa kazi zote zinakwenda kwa mujibu wa sheria kwa hivyo waandishi kama kioo cha jamii na wao wanastahiki kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na wawe mfano.
Mkurugenzi huyo amewashukuru waandishi wa habari wote kisiwani Pemba kwa mashirikiano mazuri walioipa idara yake katika utendaji wa kazi kwa mwaka 2012 na amewataka mashirikiano hayo yawe endelezwe ilikufanikisha shughuli za idara hiyo na Taifa kwa ujumla .
Aidha amewashukuru pia waandishi wa habari, viongozi wa dini pamoja na NGOs za habari kw mashirikiano walioyatoa wakati wa kutoa mawazo yao juu ya mabadiliko ya sheria No 5 ya mwaka 1988 ya magazeti na majarida Zanzibar.
No comments:
Post a Comment