Habari za Punde

Wahamiaji haramu 21 mbaroni



Na Kija Elias, Kilimanjaro
WAHAMIAJI haramu  21 kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa na
polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema walikamatwa
Januari 12 mwaka huu majira ya 7:30 usiku wilayani Same mkoani hapa.

Boaz alisema wahamiaji hao walikatwa na polisi waliokuwa doria ambapo walikutwa katika gari  lenye nambari za usajlii T 773 ALA Toyota land Cruser lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika
kwa jina la John Malamla (28).

Alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji watawafikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo wahamiaji hao ili kujibu mashitaka yanayo wakabili.


Kufutia tukio hilo kamanda huyo,alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi hilo ili kubaini mtandao wa watu wanaowaingiza nchini humo kinyume cha utaratibu kwani ni hatari kwa maisha yao.

Alisema uhamiaji haramu limekuwa tatizo kubwa mkoani hapa na kwamba, kuna
mtandao wa watu wanajihusisha na biashara ya kuwasafirisha kutoka Kenya.

Alisema watu hao hawawezi kupita mpakani na kuingia mkoani bila kuwa na watu wanaowaongoza, na kwamba wanachokifanya ni kuchunguza mtandao mzima wa watu wanaowaingiza nchini kinyume cha sheria za uhamiaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.