Habari za Punde

Watu 18 wanusurika baada ya nyumba kuungua moto

 
 
Wananchi wakisaidia kuzima moto huo.
Vitu vilivyoteketea kwenye stoo ambako kulikuwa na mita ya umeme pamoja na jiko la umeme ambalo wakazi wa nyumba hiyo wamedai kutolitumoa jiko hilo.

 
Viongozi wa Shehia ya Shangani wakikagua halihalisi ya tukio.
 
Picha na maelezo na Martin Kabemba.
 
Watu 18 wa familia 4 ya Imtiaz Kassim Yakub Dada wamenusurika kifo katika janga la moto uliotokea jana saa 5 asubuhi kwenye nyumba na.424 mtaa wa Sokomhogo, Mjimkongwe wa Zanzibar.
 
Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana ulianzia kwenye stoo, umeteketeza vitu vilivyokuwa vimehifadhiwa humo ambavyo thamani yake bado kujulikana, ulizimwa mapema kwa msaada wa Hoteli ya Marumaru ya mjini Zanzibar muda mfupi kabla ya Zimamoto kuwasili kwenye tukio hilo.
Zimamoto wametoa pongezi kwa uongozi wa hoteli hiyo chini ya Meneja wake mkuu, Prithvi Olivier Spears kwa kutoa huduma ya kwanza huku wakitumia vifaa vyao vya hoteli.

2 comments:

  1. Mkuu asante kwa hizi picha za tukio.Kama tungepata picha ya nje ya hili jumba basi ingekuwa poa zaidi.

    ReplyDelete
  2. Ahsante Mkuu

    Picha hizi sikupiga mimi nimeletewa na Mpiga picha wa kujitegemea Martin Kabemba

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.