Na Bakar Mussa, Pemba
MTU mmoja alietajwa kwa jina
la Faki Juma Faki (60) mkaazi wa Kangagani Wete, amekutwa amekufa katika ufukwe wa bahari ya Mjini Kiuyu Mkoa
wa Kaskazini Pemba.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yahya Rashid Bugi alisema
marehemu aliondoka kwake tarehe 23
mwezi huu majira ya saa moja asubuhi, kwenda kuvua uvuvi wa miguu na hakurudi tena
hadi maiti yake ilipokutwa ufukweni.
Bugi, alieleza marehemu
ambae alikuwa na maradhi ya kuanguka alipotea baharini ambapo watu wake wa
karibu walimtafuta bila mafanikio.
Daktari Abdalla Omar Hassan,
alieifanyia uchunguzi maiti, alisema kifo chake kimesababishwa na kunywa maji
mengi.
Bugi aliwataka wavuvi kuacha
tabia ya kwenda kuvua peke yao hasa wakati huu wa upepo.
Wakati huo huo nyumba moja
ya Faki Juma Rashid (35) mkaazi wa Wingwi Mjananza, imeunguwa moto na
kusababisha hasara kubwa ambayo thamani yake haijapatikana.
Kamanda Bugi, alithibitisha
kutokea moto huo na kueleza chanzo cha moto huo ni mke wa Faki kusafisha jaa la
nyumba yao na kuchoma moto takataka hizo zilizokuwa karibu na choo cha makuti
na kusababisha moto kuripuka.
No comments:
Post a Comment