Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Dk. Rawya Saud Al Busaid, wakiponyeza kitufe cha komputa kuashiria uzinduzi wa mpango wa kuwasaidia Wazanzibar katika Elimu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu wa Sultan Qaboos, uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna, akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa mpongo wa kuwasaidia Wanafunzi wa Zanzibar katika Elimu ya Juu kupitia Mfuko huo, ambao utawanufaisha Wananchi wa Zanzibar kupata ufadhili kupitia mfuko huo.
Waziri wa Elimu ya Juu Oman Dk. Rawya Saod Al Busaid, akitowa maelozo ya Mfuko huo katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena Zanzibar.koshoto Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna na kulia Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zahra Ali Hamad.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Udhamini wa Sultan Qaboos Academic Fellowship(SQSF) Hamad Al- Balushi, akitowa maelezo ya udhamini wa mfoko huo kwa Wanafunzi watakaokolifai kupata udhamini kupitia mfuko huo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika katika hoteli ya Serena Shangani Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Amina Khamis Shaban, akitowa maelezo kuhusiana na mafunzo hayo.na fursa za kupata nafasi hizo kwa kozi mbalimbali na vigezo vyake kwa waombaji.
Vice Chancellor wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Prof. Idrisa A Rai, akihutubia katika mkutano huo na kutowa maelezo ya Chuo chake katika mkutano wa iuzindizi wa mponga wa kutowa udhamini kwa Wanafunzi wa Zanzibar katika Elimu ya Juu.
Viongozi wakimsikiliza Prof. Rai akitowa maelezo ya Chuo cha SUZA.
Waandishi wakiuliza maswali baada ya uzinduzi wake.
Prof.Rai, miongoni mwa vichwa vichache Z'bar inavyoweza kujivunia.
ReplyDeleteAmeibadilisha sana SUZA baada ya wafuasi wa siasa chafu kuivuruga.
Huyu jamaa anafanana sana na akina Mahadhi Juma Mwalimu na Hamad yussuf Masauni(aliyekua mwenyekiti wa UVV-CCM)ambae kwa bahati mbaya baada ya kurudi Z'bar naona 'wazee'washaanza kumvuruga!
sina uhakika na unayosema , ila kuhusu hizi fellowship watapeana wenyewe kisiasa na kindugu kama kawaida walalahoi hawataambulia chochote hata wakiwa magenius , hili ndilo tatizo letu huko znz na tngk , kudhulumiana tu huku kujidai kuanza hotuba kwa kumtaja Mungu kama vile ni waadilifu kweli kweli , rushwa tu eeenh!
ReplyDelete