Na Othman Maulid
NAIBU
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi Gavu, ametembelea uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume kuangalia ujenzi wa maegesho ya ndege na njia ya kuondokea ndege
inoyojengwa na kampuni ya ujenzi ya Sogea Satom.
Wakati
wa ziara hiyo ameangalia maendeleo ya ujenzi wa ukuta wa uwanja ambao ujenzi
wake tayari umeshafikia hatua kubwa na karibu kilomita 7 zimeshajengwa ukuta
huo ambao unaimarisha ulinzi katika eneo la uwanja.
Naibu
Waziri alisema ujenzi wa uwanja ni moja ya kuuimarisha utoaji huduma zake na
kufikia kiwango cha kimataifa na kupokea wasafiri wengi zaidi baada ya ujenzi
wake ambao utachukuwa miezi 18 kukamilika.
Baada
ya maegesho hayo kukamilika yatakuwa na uwezo wa kutoa huduma za ndega nane
kubwa aina ya boeing 767.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar, Said Iddi Ndumbogani
alisema ujenzi huo utahusisha eneo la maegesho ya ndege na njia ya kuondokea
ndege katika uwanja huo.
Mkurugenzi
huyo alisema ujenzi huo utagharibu zaidi ya dola milioni 57 hadi kukamilika
kwake.
Alisema
kwa sasa wanaweza kuhudumia abiria zaidi ya 1000 kwa wakati mmoja katika uwanja
huo na kuweza kutoa huduma za maegesho ya ndege zaidi ya tano.
No comments:
Post a Comment