Habari za Punde

Ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar.

 Msimamizi wa Minara ya Kuongozea Meli ya Shirika la Bandari Zanzibar Juma Hassan akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Gavu, jinsi ya matumizi ya gesi kwa ajili ya kutowa mwaka katika mnara kuonekana na Meli zinazopita katika ukunda wa bahari ya Zanzibar kupitia Mnara wa Nungwi ulioko Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Msimamizi wa minara ya kuongezea  meli akitowa maelezo ya uwakaji wa alama ya taa katika mnara huu..
Mnara wa Nungwi unavyoonekana Pichani.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Mhe. Issa Haji Gavu akiangalia taa ya mnara wa Mwangapwni alipokuwa na ziara ya kutembelea minara ya kuongozea meli Zanzibar.
Msimamizi wa Minara ya Kuongozea Meli ya Shirika la Bandari Zanzibar Juma Hassan akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar Issa Haji Gavu,akimsikiliza msimamizi huyu akitowa maelezo ya mnara wa Makunduchi Unguja Mkoa wa Kusini Unguja.unaotumiwa na meli mbalimbali zinazopita ukanda huo kuziongoza Meli..


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.