Na Fatma Kassim, Maelezo
WIZARA ya Afya imeanza kutoa chanjo ya kinga
ya maradhi ya nyumonia, homa ya uti wa
mgongo na kuharisha kwa watoto kuanzia
wiki sita katika hospitali na vituo vya afya Unguja na Pemba.
Kwa mujibu wa tarifa zilizotolewa na Kaimu Mratib
wa kitengo cha chanjo, Abdulhamid Ameir Saleh alisema katika kufanikisha chanjo
hiyo mpya kitengo hicho kimejipanga vyema katika kuwapatiwa watoto wote
wanaostahiki chanjo hiyo.
Alifahamisha kuwa dawa za kutosha kwa kipindi cha miezi sita mwanzo
tayari zipo ambapo kiasi ya shilingi
milioni 300 zimetumika kupatikana kwa
dawa hizo zilizotolewa na shirika la kimataifa la Gavi pamoja na serikali ya Tanznaia.
Alisema
chanjo hizo zitatolewa kwa kila mtoto anaezaliwa kwa kipindi hichi na ni salama na tayari zimeshatolewa katika nchi kadhaa duniani kwa
lengo la kutokomeza magonjwa hayo yanayoongoza kuchangia vifo kwa watoto chini
ya miaka mitano.
Amewataka wananchi kuwapeleka watoto wao
katika vituo vya afya kupata chanjo hiyo
mpya.
No comments:
Post a Comment