Wananchi wa eneo la Daraja Bovu wakimuangalia Kijana aliyepata ajali katika barabara hiyo wakati akiendesha Vespa yenye namba za usajili Z 728 CB, akitokea Mtoni kidatu na kuelekea Amani, aligongana na gari aina ya Toyota ikiwa na Wafanyakazi wa hoteli ya Lagema Nungwi.
Vespa aliyopata nayo ajali ikiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo. Kuna Vijana siku hizi hutumia vespa kuonesha manjonjo na kwenda mwendo wa kasi na kuzipita gari kwa mwendo wa kasi wakiwa wanafukuzana.
Kijana Muhidini Ali Ame akiwa amelazwa katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja, baada ya kupatiwa matibabu akiwa katika wodi ya wagonjwa wa ajali akiendelea na matibabu katika hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment