Bandari ya Boti za Kwenda Dar - es - Salaam ikiwa katika kiwango cha Kimataifa baada ya kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu ili kuwa na kiwango hicho kwa abiria wanaotumia bandari hiyo wanapoingia Zanzibar na kutoka.
Hii ni sehemu ya kukaa abiria wanaposubiri boti na kujikinga na Mvua na Jua ambayo imefanyiwa ujenzi huo na Kampuni ya Azam Marine , ili kutowa huduma kwa wateja wa Azam, bado inaendelea na ujenzi wa sehemu ya Daraja la Kwanza
Majengo ya Daraja la Kwanza kwa Abiria wa Kampuni ya Azam Marine yakiwa katika ujenzi wake wa hatua ya mwisho ili kutowa huduma hiyo kwa abiria wao wanaotumia Boti zao za Kilimanjaro.
Hongera Bakhresa na Smz , hii ndo mifano ya kuigwa , wengi wanasema kauziwa Bakhresa n.k , kwa mtizamo wangu bora zimwi likujualo....angepewa mzungu / mgeni angekusanya pesa na kuondoka....ATCL , TTCL , IPTL/ TANESCO n.k
ReplyDeleteyap yap mdau hapo juu umeongea zimwi likujualo halikuli likakwisha na mchawi mpe mwanao alee ataogopa kumdhuru maana atakipaka
ReplyDeleteShabash Hivi ndivo ilivotakiwa hata kule Airport ya Zanzibar kuwe na Turnel za wageni wanaoingia na kutoka. Ahsante sana ndugu Othman kwakutuletea picha kama hizi. Kwani zinatia moyo na hamu yakutaka kusaidia.
ReplyDeleteTurnel hii yakuingia na kutoka DSM inatakiwa wawekwe Wazanzibar ambao wataweza ku-control Immigration. Kama tunavyojua kuna watu wengi ambao wanamiminika katika Visiwa vyetu. Na wengi wao hatujui usalama wao uko vipi.
kuwa na sehemu hii ni moja yakuweza kuwa na udhibiti wa Waingiao kama wote wana sifa za kuingia Visiwani. Ningeomba na ile Bandari ya Nungwi. na ile ya Dunga zifanyiwe ukrabati na kuwe na udhibiti Mzuri wa Uingiaji wa watu Visiwani.
Mbona Dunga hakuna bandari umekusudia wapi alhabiby
Deletehahahaaaa eti bandari ya Dunga mie naona amekusudia Fumba maana kwenye keybord F-D ziko karibu labda vidole vimekosea na sio kama haijuwi jiografia ya zenji msamehe kwa hilo
ReplyDelete