Habari za Punde

Bandari ya Zanzibar ya Boti za Dar -es- Salaam Waaaaa.............

Bandari ya Boti za Kwenda Dar - es - Salaam ikiwa katika kiwango cha Kimataifa baada ya kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu ili kuwa na kiwango hicho kwa abiria wanaotumia bandari hiyo wanapoingia Zanzibar na kutoka.
Hii ni sehemu ya kukaa abiria wanaposubiri boti na kujikinga na Mvua na Jua ambayo imefanyiwa ujenzi huo na Kampuni ya Azam Marine , ili kutowa huduma kwa wateja wa Azam, bado inaendelea na ujenzi wa sehemu ya Daraja la Kwanza  

 Majengo ya Daraja la Kwanza kwa Abiria wa Kampuni ya Azam Marine yakiwa katika ujenzi wake wa hatua ya mwisho ili kutowa huduma hiyo kwa abiria wao wanaotumia Boti zao za Kilimanjaro.

5 comments:

  1. Hongera Bakhresa na Smz , hii ndo mifano ya kuigwa , wengi wanasema kauziwa Bakhresa n.k , kwa mtizamo wangu bora zimwi likujualo....angepewa mzungu / mgeni angekusanya pesa na kuondoka....ATCL , TTCL , IPTL/ TANESCO n.k

    ReplyDelete
  2. yap yap mdau hapo juu umeongea zimwi likujualo halikuli likakwisha na mchawi mpe mwanao alee ataogopa kumdhuru maana atakipaka

    ReplyDelete
  3. Shabash Hivi ndivo ilivotakiwa hata kule Airport ya Zanzibar kuwe na Turnel za wageni wanaoingia na kutoka. Ahsante sana ndugu Othman kwakutuletea picha kama hizi. Kwani zinatia moyo na hamu yakutaka kusaidia.

    Turnel hii yakuingia na kutoka DSM inatakiwa wawekwe Wazanzibar ambao wataweza ku-control Immigration. Kama tunavyojua kuna watu wengi ambao wanamiminika katika Visiwa vyetu. Na wengi wao hatujui usalama wao uko vipi.
    kuwa na sehemu hii ni moja yakuweza kuwa na udhibiti wa Waingiao kama wote wana sifa za kuingia Visiwani. Ningeomba na ile Bandari ya Nungwi. na ile ya Dunga zifanyiwe ukrabati na kuwe na udhibiti Mzuri wa Uingiaji wa watu Visiwani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona Dunga hakuna bandari umekusudia wapi alhabiby

      Delete
  4. hahahaaaa eti bandari ya Dunga mie naona amekusudia Fumba maana kwenye keybord F-D ziko karibu labda vidole vimekosea na sio kama haijuwi jiografia ya zenji msamehe kwa hilo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.