Habari za Punde

KMKM Yaendelea kutesa Ligi Kuu ya Zanzibar baada ya kuifunga Mtende Rengers 3--0

 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Wilaya ya Mjini  ZFA Hassan Chura na viongozi wengine wakifuatilia mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kati ya timu ya Mtende Rengers na KMKM, uliofanyika uwanja wa Amaan, na timu ya KMKM kutoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-0 na kuendelea kuongoza Ligi hiyo.   
 Mchezaji wa KMKM kushoto Haji Simba na kulia Abdulhalim Abdalla, wakiwania mpira katika mchezo huo wa ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa Amaan, timu ya Kmkm imeshinda 3--0 
 Mchezaji wa KMKM Kassim Abdukadir Nemshi akimpita beki wa timu ya Mtend Rengres Abdulhalim Abdalla, ka tika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar.


 Benchi la Wachezaji wa timu ya Mtende Rengers wakiwa na majozi wakati wakifuatilia mchezo wao na timu ya KMKM uliofanyika uwanja wa Amaan na kubugia kichapo cha mabao 3--0 
Waandishi wa habari wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar kati ya Mtende Rengers na KMKM, uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Kmkm imeshinda kwa mabao 3--0.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.