Habari za Punde

Mabingwa Kombe la Dk. Shein Mkoa wa Kaskazini Unguja Yapongezwa kwa Ubingwa huo.

Nahodha wa Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja akimkabidhi kombe cha ushindi Rais Mstaafu wa SMT Mzee Ali Hassan Mwinyi baada ya timu hiyo kuchukuwa Ubingwa wa Michuano  ya Dr. Shein Cup yaliyofanyika wakati wa sherehe za kutimia  miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan..
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya mchezaji wa timu ya Mkoa wa Kaskazini mkoba uliokuwa na viatu akipokea kwa niaba ya Wachezaji wezake, baada ya kuowa Kombe la Dk. Shein, liloshirikisha timu za Mikoa yote ya Zanzibar  tibeba viatu mmoja wa wachezaji wa Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja katika hafla ya kuwapongeza kwa ushindi huo hapo Pwani mchangani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi shilingi Milioni 3,500,000/- kwa wachezaji wa Timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini unguja iliyopata ushindi katika mashindano ya Dr. Shein Cup.Zawadi hiyo kila mchezaji alipata shilingi 50,000/-.


Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wachezji wa timu ya Soka ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyochukuwa ubingwa wa mashindano ya Dr. Shein Cup.Kulia ya Mzee Mwinyi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na kushoto ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji na Mmoja wa waliofadhili mashindano hayo Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza.(Picha na Hassan Issa OMPR – ZNZ.)

4 comments:

  1. Mh,raza miguu inafunza nini?naona viatu huviwezi

    ReplyDelete
  2. watu wazima karibu kuingia makaburini , nchi imekushindeni kuipatia mahitaji muhimu mnabakia kucheza mpira , majukumu muhimu ya nchi kama maji, umeme, elimu na afya mmeyapiga chenga ..........

    ReplyDelete
  3. NDUGU YANGU lawama hazina maana kila jamba lina utaraibu wale na matatizo ya jamii hutatuliwa na jamaii. Serekali iko katika mikakati ya kutatua matatizo yote ya wananchi kwa awamu na tatizo la umeme loko njiani kumalizika mungu akipenda mwezi huu tatizo hilo lotakwisha.kuhusu elimu hali kadhalika na mengine, usiwe wa kulaumu onesha mfano wa kutowa mawazo yako kuliko kutowa dosari hata wewe huwezi kuziondowa.

    ReplyDelete
  4. miaka zaidi ya 50 mapinduzi dhuluma, tumejitawala nini? kama huduma muhimu zinatushinda si bora tungeendelea kutawaliwa na wakoloni? utaratibu gani unaozungumzia ndugu yangu usie na shule? miaka 50 kidogo? kwa ajili ya kupatia maji na umeme nchi ndogo kuliko hata robo ya mkoa wa dar es salaam? hivi unafikiri? au unataka sifa kwa serikali ya majambazi na chama cha majambazi ( CCM ) anayetoa dosari ndie mwenye mapenzi na wewe muogope mwenye kukusifu hakutakii maendeleo. Dosari hizo zinaweza kuondolewa mara moja tu ukivunjika muungano haramu wa tanzania , kama huamini wache muungano uvunjike uone.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.