Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Atembelea eneo la Tukio.

 MAKAMU wa Pili  wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Uongozi wa skuli ya Kijitoupele wakati alipofika katika eneo la bonde la mpunga la kijitoupele alipozama mwanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli hiyo, Naifat Abdalla Mrisho jana.
MWALIMU Mkuu wa Skuli ya Kijitoupele ‘A’, Saada Rajab Ali akitoa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati makamu huyo alipofika eneo la bonde la mpunga la Kijito upele alipozama mwanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli hiyo, Naifat Abdalla Mrisho jana.

1 comment:

  1. mpaka mtu atoke roho ndio mchukue hatua ? basi mtambue wote wanaohusika na kifo cha mtoto huyu watasimama mbele ya Mola kujibu masuala mazito , kiongozi sio maana yake kuishi kwenye jumba zuri, kuendeshwa kwenye gari zuri na kulindwa na maaskari kama vile unatafutwa kuuawa , bali ni kutatua matatizo ya raia , usalama wao na mahitaji muhimu ya maisha. Hii roho ya mtoto huyu itawaandama viongozi wote wahusika waliozembea.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.