Mbunge wa Jimbo la Magomeni Mohammed Amour Chombo akitoa nasaha kwa wanafunzi,na pia kuwapongeza kwa kufaulu kwao kabla ya kuwazawadia sare za Skuli kwa kila mwanafunzi,huko katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.)
Na Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar .16/3/2013.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin amewataka wanafunzi wa jimbo hilo kuengeza juhudi katika masomo yao ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Aliyasema hayo Jana huko katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere wakati akitoa zawadi za sare za skuli kwa wanafunzi waliofaulu masomo yao .
Alisema kuwa wanafunzi wa jimbo hilo wajitahidi kadri ya uwezo wao wasome kwani mambo mengine hayana maana yanadumaza elimu.
“Mambo ya watoto bandia muyaache kwani hayana maana katika elimu elimu ni ufunguo wa maisha msijaribu kuupoteza”. .Alisema Salmin.
Aidha alisema kuwa katika skuli ya sekondari ya nyerere kunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa walimu wa sayansi jambo ambalo litawasababishia wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo hayo.
Nae mbunge wa jimbo hilo Mohammed Amour Chombo aliwapongeza wanafunzi hao na kuwataka kutafakari nasaha ambazo wanazopewa na kusema kuwa hakuna jambo zuri kama kusoma .
Alisema kuwa bila ya elimu hutoweza kupata ajira katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Aidha aliwataka wanafunzi hao wawe wasikivu kwa wazee wao ili waweze kuwa waadilifu “bila ya kuwasikiliza wazee wenu basi mtaharibikiwa ” Alisema Chombo.
Alisema kuwa wanafunzi muyasikilize kwa makini maneno mnayoambiwa na muyatafakari ili muweze kuyatekeleza kwa vitendo kwa maslahi yenu na vizazi vyenuZaidi ya shiling millioni tatu zilitumika kwa kununulia sare za skuli kwa wanafunzi hao waliofaulu na ni jumla ya wanafunzi 198 wanawake na 183 wanaume
No comments:
Post a Comment