Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Same, Mhashamu Rogati Kimario (pichani) ametoa wito kwa
Wakristu wa Zanzibar kusimama imara kwa magumu yote yanayo wakabili katika maisha yao na kuongeza kuwa
katika Msalaba wa Yesu Kristu, kuna siri kubwa ya upendo na msamaha . Askofu Rogati pia amewahimiza kusali kwa bidii kuliombea Taifa letu la Tanzania amani na utulivu.
Askofu Rogati alisoma Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Minara miwili mjini Zanzibar kutoa mkono wa pole kwa msiba wa Padri Evarist Mushi kutoka kwa waumini wa Jimbo lake la Same, Tanzania Bara.
Picha na Martin Kabemba
No comments:
Post a Comment