Ujumbe wa Manispaliti ya Kiruna ukiongozwa na Bwana Ove, watatu kutoka kushoto, wakimsubiri kwa hamu Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, afisini kwake.
Manispaliti ya Kiruna imeanzisha uhusiano na wadi za Makunduchi mwaka 2011. Chini ya makubaliano hayo elimu na utalii unaojali mazingira umetiliwa maanani.
Wanafunzi wanawake wapatao 12 kutoka kila shehia ya Makunduchi watapatiwa mafunzo ya mienzi minne katika kiingereza, ujasiliamali na kompyuta. Kila mwanafunzi atakuwa na mwalimu mmoja kutoka Kiruna.
Wanafunzi watatu watakaofanya vizuri watapatiwa nafasi ya kwenda Kiruna kwa mafunzo zaidi. Ujumbe huu wa watu 10 (wengine hawapo pichani) utakuwepo nchini kwa siku nne kwa ajili ya kupanua maeneo mengine ya ushirikiano.
Eneo la maji litapewa kipaumbele katika mashirikiano ya sasa. Katika picha upande wa kulia ni afisa tawala wa Wilaya ya Kusini akifuatiwa na bwana P.G Idivuoma, mwengine ni bwana Keneth Stalnacke ambaye alikuwa meya wa Kiruna.
Mwanamke ni Bi. Johanna Ericson ambaye atakuwa mwalimu mkuu wakati wa mafunzo yatakapoanza. Uhusiano wa Kiruna na Wadi za Makunduchi unatokana na juhudi za Wadi zenyewe za kutafuta maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment