Habari za Punde

Vodacom Yatoa Misaada Soba House Zenj

Mfanyakazi wa Vodacom Afrika Kusini Musa Nkuna na Nuru Ntisi wa kituo cha kusaidia wanawake kuachana na  matumizi ya Dawa za Kulevya cha Mjini Zanzibar (Soba House) akiwa na mwenzake Amina Salum (wa tatu kushoto) wakifurahia makabidhiano ya  vyakula na vitu vingine mbalimbali vilivyotolewa na Vodacom Foundation. Wengine pichani ni wafanyakazi wa  Vodacom Afrika Kusini na wenzao wa  Tanzania walipojumuika kwa pamoja kukitembelea kituo hicho  kama sehemu ya kuwatia moyo kutimiza azma ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania pamoja na wenzao wa Afrika Kusini wakiwa wamejumuika na wateja wa kituo cha kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sobber House) cha wanawake cha Mjini Zanzibar wakati wafanyakazi hao walipokitembelea kituo hicho na kutoa msaada wa vyakaula na vitu mbalimbali ili kuwapa moyo wanawake hao walio katika harakati za kuachana na matumizi ya dawa za kulevya kufikia azima yao.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (aliyechuchumaa kushoto) akitoa maelezo ya zawadi ambazo kitengo chake kimeipatia kituo cha kutibu wanawake kuchana na matumizi ya dawa za kulevya cha Mjini Zanzibar wakati kundi la wafanyakazi wa Vodacom Afrika Kusini walipoungana na wenzao wa Tanzania kutembelea kituo hicho kama sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wa kituo hicho kusaidia wanawake Mjini Zanzibar.
Mlezi wa Kituo cha Kusaidia wanawake kuchana na Matumizi ya Dawa za Kulevya cha Mjini Zanzibar Mama Fatma Sukwa(katikati), Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(kulia) na Mteja wa kituo hicho Monica Pardo amabe ni Rais wa Uhispania ambaye yuko katika kituo hicho  wakiwa katika picha ya kumbukumbu wakati kundi la wafanyakazi wa Vodacom Afrika Kusini walipojumuika na wenzao wa Tanzania kukitembela kituo hicho na kukipatia msaada wa vyakula na vitu vingine mbalimbali.

Wafanyakazi wa Vodacom Musa Nkuna wa Vodacom Afrika Kusini (kushoto) na Salum Mwalim wa Vodacom Tanzania(Kulia) wakiwa hoi na mapozi ya Jacqueline Samson wa kituo cha kuachana na matumizi ya dawa za kulevya cha wanawake cha Mjini Zanzibar akiwa amejipamba na mkufu uliotengezewa kwa punje z amaharage na karatasi ikiwa ni kazi z amikono za wanawake wanaopata tiba kituoni hapo huku baadhi ya wafanyakazi wengine wa Voidacom Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kuipata picha ya Jacquline. Wafanyakazi wa Vodacom walitembelea kituo hicho na kukabidhi msaaada wa vyakula na vitu vingine mbalimbali kuunga mkono juhudi za kituo hicho.
Wafanyakazi wa Vodacom Afrika Kusini na wenzao kutoka Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  na viongozi pamoja na wateja wanaopata tiba katika kituo cha kutibu wanawake lkuachana na matumiiz ya dawa za kuelvya. Wafanyakazi hao wlaikitemebela kituo hicho kama sehemu ya kuthamini juhudi za kituo hicho kusaidia wanawake kuachana na matumizi ya dawa hizo za kulevya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.