Wanafunzi wa skuli ya Kusini wakiwa nje ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Sweden kwa ziara ya kimasomo. Skuli ya kusini iliyoko Makunduchi imeanzisha uhusiano na Skuli iitwayo Sundsvall ya Sweden.
Katika uhusiano huo ulioanza mwaka jana wanafunzi pamoja na walimu wa Sundsvall wameshawatembelea wenziwao Skuli ya Kusini mara mbili. Katika uhusiano huu walimu wa skuli ya Kusini watajifunza mbinu za kisasa za ufundishaji kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ICT.
Skuli za Makunduchi zimo katika harakati za kutafuta njia bora za ufundishaji kufuatia ufaulu mbaya katika mitihani ya taifa uliozikumba skuli nyingi hivi karibuni hapa nchini.
Wakiwa nchini Sweden walimu wa skuli ya Kusini watajifunza mbinu wa kufundisha kwa kutumia njia ya mawasiliano ICT ili kupambana na tatizo la ufaulu mdogo uliozikumba skuli nyingi hapa nchini.
Katika picha wa kwanza kutoka kushoto ni mwalimu Juma Ali Simai ambaye ni mratibu wa safari hiyo, na wa kwanza kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu ndugu Shamsi Ameir.
Uhusiano huu ulioanzishwa ni kutokana na jitihada za walimu wenyewe wakisaidiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Mzuri Kaja (Mzuri Kaja Development Society - www.mzuri-kaja.or.tz)
Sijawahi kusikia mahusiano kama haya kwa skuli za Pemba.Sijui haya mahusiano yanapatikana vipi Unguja yasifike Pemba
ReplyDeleteMdau Mawasiliano kama hayo yanategemea Uongozi wa Skuli husika kufanya urafiki na skuli za nje kwa kupitia kwa barua na propozo za kuomba ushirikiano wa kimasomo na skuli husika au nchi husikandivyo inavyopatikana kaka na kama na wewe unataka mambo haya jaribu kutafuta marafika katika mitandao na utafanikiwa kama walivyofanikiwa hawa wa skuli ya Makunduchi.
ReplyDeleteHapa Nakunga mkono Kaka Mapara Binafsi niliwahi kuwanganishia baadhi ya maskuli pamoja na vijana wanaofanya michezo ya aina mbali mbali huko zanzibar wafanye urafiki wa aina hiyo katika nchi za skandenevia lakini matatizo ya nyumbani ni kutokuwa na watu makini
ReplyDelete