Habari za Punde

Ziara ya ujumbe wa Manispalit​i ya Kiruna Sweden huko Makunduchi

 Ujumbe wa Kiruna ukifurahia utamaduni wa watu wa Makunduchi siku ya utamaduni wa pande hizo mbili.
 Wamasai nao walialikwa kuja kuonyesha utamaduni wao ambao unafanana na ule wa kabila la Sami kutoka Kiruna.
 Watu wa Makunduchi waliwaonyesha wageni wao jadi ya Shomoo hapo katika kiwanja cha Skuli ya Makunduchi.
Bi Sari, mjumbe wa Manispaliti ya Kiruna akiwatumbuiza wakaazi wa Makunduchi wakati wa maonyesho ya utamaduni yaliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Makunduchi. Bi Sari anatoka katika kabila la Sami ambalo linaishi kama wamasai, kuhamahama na mifugo yao. Watu wa kabila la Sami wameenea Kaskazini ya Nchi za Skandanavia.
 
Wakaazi wa Makunduchi wakionyesha utamaduni wao wa kupigana makoa wakati wa siku ya utamaduni wa Kiruna na Makunduchi hapo Skuli ya Makunduchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.