Habari za Punde

Ziara ya ujumbe wa Manispalit​i ya Kiruna Sweden yamalizika kwa kutoa misaada mbali mbali

Ziara ya ujumbe wa Manispaliti ya Kiruna Sweden yamalizika kwa kutoa misaada kwa skuli za maadalizi za Makunduchi. Kwenye picha Bi. Sofie kutoka Save the Children akimkabidhi vifaa mbali mbali vya kuchezea watoto mwalimu Ameir Haji Ameir maarufu Kuo kwa ajili ya Skuli ya Maadalizi ya Kajengwa ambayo ilikuwa katika hali mbaya mno kuliko.

Mwalimu Ameir akipokea busati kwa ajili ya kukalia watoto wa skuli ya maadalizi ya Kajengwa.

Mwenyekiti wa ushirikiano baina ya wadi za Makunduchi na Manispaliti ya Kiruna Mwalimu Mwita Masemo akipokea Bendera ya Kiruna kutoka kwa mwanasiasa wa Kiruna bwana P.G Idiovum wakati wa Sherehe ya kuangana iliyofanyika katika hoteli ya La Madrugada Kigaeni Makunduchi

Mwalimu Mwita Masemo akitoa zawadi ya embe kwa Bwana P.G wakati wa kuagana. Makunduchi ni maarufu kwa kutoa embe tamu hapa Zanzibar.


Walimu wa skuli za maandalizi wakigawana zawadi zilizotolewa na ujumbe wa Manispaliti ya Kiruna ambao umemaliza ziara ya siku 4 Makunduchi

Ujumbe wa Manispaliti ya Kiruna wapiga picha ya pamoja na wenyeji wao Wadi za Makunduchi.
Waliokaa kitako ni wanafunzi waliochaguliwa kujifunza kompyuta, ujasirimali na kiingereza. Masomo hayo yanategemewa kuwa ya mwaka mmoja badala ya mienzi minne kama ilivyoripotiwa awali. Mstali wa pili waliosimama wa saba kutoka kushoto ni afisa tawala wa Wilaya ya Kusini Unguja, ndugu Abdallah Kombo



1 comment:

  1. Pamoja na misaada kama hiyo pamoja na mashirikiano na wenzetu hawa, tunapaswa tuwe makini sana, kwani wenzetu wana mitazamo ya mbali sana, wana malengo zaidi ya huo ushirikiano. Nina wasiwasi na suala la kuharibu maadili kisirisiri bila sisi kujijua, kwani wameingia kwenye jamii mnoo, kwa kweli tuwe makini mno,
    sipingi mashirikiano na wenzetu hao lakini uzoefu unaonesha mara nyingi sisi huwa ndio waathirika pamoja na misaada mbalimbali.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.