Habari za Punde

Boresha Elimu Skuli ya Kusini yazidi kujipanga

 Ramani ya maabara yenye vitengo vitatu, kemia, biologia na fizikia
 Ramani ya madarasa mawili ya kisasa yatakayoku​wa na 'fixed projector' Mradi huu utatekelezwa baada ya kumalizika mradi wa maabara
 Ramani ya chumba cha Kompyuta na Maktaba

 
Mwalimu Rashid Shamsi kutoka kushoto na ndugu Hassan maarufu Kijundu ambaye ndiye Mkuu wa Ujenzi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mzuri wakitafakari kazi iliyo mbele yao ya kutekeleza miradi mitatu ya elimu iliyobakia. Ndugu Hassan ni 'marine engineer' anayefanyakazi kitengo cha cherezo Bandarini. Mwalimu Rashid ni mmiliki wa shule ya ushonaji The Modern Tailoring Academy iliyopo Magomeni
 Miongoni mwa shamra shamra za ufunguzi wa nyumba ya walimu, mgeni rasmi alitunuku vyeti kwa wasamalia wema waliochangia ujenzi wa nyumba ya walimu. Cheti hiki kilipokelewa na ndugu Muombwa kwa niaba ya Amie Bishop na familia yake. Bi Amie ni raia wa Marekani ambaye amekuwa alichangia kiasi cha shilingi milioni 10 kuendeleza ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo imejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 100.
Jengo la nyumba ya walimu linavyoonekana baada ya ufunguzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein.
 
Kumalizika kwa jengo hili kumetoa nafasi kwa Jumuia ya Maendeleo ya watu wa Mzuri (Mzuri kaja Development Society) kuanza kwa mradi wa ujenzi wa Maabara ya kisasa itakayokuwa na vitengo vitatu, kitengo cha kemia, biologia na fizikia.
 
Kumalizika kwa maabara kutafungua mlango mwengine wa kuanzisha mradi wa madarasa ya kisasa mawili. Mradi huu nao utafuatiwa na mradi mwengine wa chumba cha kompyuta na maktaba.
 
Kwa kifupi Jumuiya ya Maendeleo ya watu wa Mzuri inayojumuisha wanachi wote wenye itikadi tofauti imekusudia kuleta mageuzi ya elimu katika Skuli ya Kusini, Makunduchi chini ya mpango wa miaka 15 wa kuboresha miundo mbinu ya elimu. Mpango huu unaitwa Boresha Elimu Skuli ya Kusini.
 
Jumuiya imekusudia kuachana kabisa na siasa chafu za visiwani zisizokwisha pamoja na kuachana kabisa na wanasiasa wanaotumia migongo ya wananchi kupata vyeo na badala yake kushughulikia elimu kwa wote.
 
Jumuiya inatoa wito kwa kila mwenye kutaka kutoa misaada isiyokuwa na masharti kuwasiliana na Mratibu, ndugu Muombwa 0773539504 mmuombwa@hotmail.com Nyote mnakaribishwa. Ahsanteni

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.