Habari za Punde

Breaking News - Msanii Mkongwe wa Muziki wa Taraab Zanzibar Haji Mohammed Amefariki Dunia asubuhi hii Hospitali ya Muhimbili


Habari tulioipata sasa hivi kuwa Msanii Mkongwe na Muziki wa Taraab wa  Kikundi cha Taraab cha Melody East  Africa  Haji Mohammed Kijikuu cha Siti Bint Saad, amefariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Muhimbnili baada ya kuzidiwa na Presha asubuhi ya leo majira ya saa nne.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari kwa muda mrefu na presha, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa mchana huu na boti ya Kampuni ya Azam Marine saa 9.45 jioni kwa ajili ya maziko yatafanyika Mjini Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Melody Hashim Salum amesema amezungumza na marehemu asubuhi na kamwambia anakwenda hospitali kuonanana Daktari wake,, na kushtuka kupata habari ya Msiba huo majira ya saa 4,asubuhi.

Marehemu Haji Mohammed ameacha  watoto watatu.
Mungu amlaze Pema Peponi Amani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.