Habari za Punde

KMKM yawasha indiketa

 
Na Haji Nassor, Pemba
 
MABAHARIA wa KMKM, jana waliongeza kasi kuufukuzia ubingwa wa ligi kuu ya soka Zanzibar msimu huu, baada ya kuwalaza Duma mabao 2-1 katika uwanja wa Gombani, Pemba.
Katika mchezo huo, KMKM ilionesha mapema dhamira ya kutoka na ushindi kwa kuzifumania nyavu katika dakika ya kwanza tu, kwa bao lililofungwa na Mwinyi Ameir aliyeunganisha krosi ya Ame Msimu.
Hata hivyo, Duma ilijiweka sawa na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji wake Yahya Khamis.
Hadi timu hizo zinakwenda kupumua, matokeo yalikuwa sare ya 1-1, na KMKM ilirudi uwanjani kwa kasi mpya na kujipatia bao la pili katika dakika ya 61 ambalo mara hii liliwekwa kimiani na Mudrik Muhibu.
Kwa ushindi huo, KMKM imezidi kujikita kileleni mwa msimamo ikifikisha pointi 40, baada ya kucheza mechi 18, huku Duma ikiwa katika hatari ya kushuka daraja kwani hadi sasa ina pointi 17 ikiwa imecheza mechi 20.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mchezo kati ya Malindi iliyotishia kujitia, na wajenga uchumi wa Duma, ambao wote wanakabiliwa na hatari ya kuteremka daraja.

1 comment:

  1. Wakowapi wale wachezaji wa zamani wa zanzibar kama kina Mustafa Kassim, Abdulmajham, Saif Nassor, Sulaiman Othman Nyanga, Salhina maftah, Abdulhalim mapembe, Mohammed Kassim, Boti, nimesikia Maulid Mohammed (Machaprala amefariki Allah amrehemu), Ambar, Malik, Mussa Baucha, hawa nawakumbuka bado nilipokua Zanzibar during 1968.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.