Na Mwandishi Wetu
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika Azam FC, leo inashuka uwanja wa Taifa kuikaribisha klabu ya Barrack Young Controllers kutoka Liberia katika mechi ya marudiano ya mzunguko wa pili wa ngarambe hizo.
Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amekaririwa akisema kuwa, Umony amepona na amekwishaanza mazoezi na wenzake, na kwamba angeweza kumtumia hata kwenye mechi na Ruvu Shooting wiki iliyopita, lakini aliamua kumuacha apone sawasawa.
Azam inacheza mechi hiyo huku ikitarajiwa kuongezewa nguvu na mshambuliaji wake wa kimataifa, Mganda Brian Umony ambaye amepona majeraha.
Kocha wa Azam FC, Muingereza Stewart Hall amekaririwa akisema kuwa, Umony amepona na amekwishaanza mazoezi na wenzake, na kwamba angeweza kumtumia hata kwenye mechi na Ruvu Shooting wiki iliyopita, lakini aliamua kumuacha apone sawasawa.
“Alikuwa amepona kitambo na angeweza kucheza dhidi ya Ruvu Shooting. Yuko fiti kabisa na kesho (leo) anaweza kucheza”, alisema Hall.
Umony aliumia dakika ya tisa katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya michuano hiyo dhidi ya Al Nasir ya Sudan Kusini na tangu wakati huo hajagusa mpira.
Kwa upande mwengine, Hall ameelezea matumaini yake kuwa, vijana wake watatoka na ushindi katika pambano hilo, huku akisema mashabiki watakaohudhuria mchezo huo wana nafasi kubwa ya kuhamasisha ushindi huo.

“Timu iko vizuri kabisa na tunaomba wapenzi wa soka wajitokeze kwa wingi kutushangiria, tutawapa burudani nzuri na watafurahia”, alijigamba Muingereza huyo.
Azam inahitaji sare ya aina yoyote leo, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza ugenini.
Azam inahitaji sare ya aina yoyote leo, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza ugenini.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka visiwa vya Comoro
No comments:
Post a Comment