Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Hatua hiyo inafuatia maombi ya wachezaji walio kundini hivi sasa, kutaka nyota hao warejeshwe, kwa lengo la kukabiliana vyema na hatua iliyobakia katika ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya simu Vodacom.
“Wachezaji na baadhi ya watu wa benchi la ufundi wameomba hawa wawili warejeshwe. Na hata wachezaji wenyewe kwa kweli wameonesha nia ya kurejea kikosini na kuitumikia timu kwa moyo mmoja”, amesema Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga.
KLABU ya Simba huenda ikawarejesha kikosini kiungo Mwinyi Kazimoto na mshambuliaji Felix Sunzu Jr. ili kukiongezea nguvu katika mechi zake za ligi kuu ya soka Tanzania bara inayoelekea ukingoni.
Hatua hiyo inafuatia maombi ya wachezaji walio kundini hivi sasa, kutaka nyota hao warejeshwe, kwa lengo la kukabiliana vyema na hatua iliyobakia katika ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya simu Vodacom.
“Wachezaji na baadhi ya watu wa benchi la ufundi wameomba hawa wawili warejeshwe. Na hata wachezaji wenyewe kwa kweli wameonesha nia ya kurejea kikosini na kuitumikia timu kwa moyo mmoja”, amesema Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga.
Kamwaga amesema taratibu za kuwarejesha wawili hao kundini zimeanza na ndani ya siku mbili hizi wanaweza kuanza mazoezi na wenzao.
Sunzu, raia wa Zambia mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mzalendo, Kazimoto ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Simba walioondolewa kwenye programu ya timu kwa sasa kutokana na utovu wa nidhamu.
Wengine ambao kocha Mfaransa Patrick Liewig hataki kuwaona ni mabeki Juma Nyosso, Amir Maftah, Paul Ngalema, Komabil Keita kutoka Mali, viungo Ramadhani Chombo, Haruna Moshi na mshambuliaji Abdallah Juma.
Kwa sasa, Simba inaundwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili, wakiongezewa nguvu na wachache waliokuwa kikosi cha kwanza, mabeki Shomary Kapombe, Nassor Masoud, viungo Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
Tayari Simba imeshapoteza mwelekeo wa kutetea ubingwa wake ilioutwaa msimu uliopita, wakishika nafasi ya nne kwa pointi 35, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam FC 43 na Yanga walio kileleni kwa pointi 49.
No comments:
Post a Comment