Habari za Punde

Kikosi cha PBZ kukipiga na Timu ya Masharobaro wa Saloon Zanzibar Uwanja wa Amaan.leo.

Kikosi kazi cha timu ya PBZ Zanzibar kutowa Elimu kwa timu ya Umoja wa Saloon Zanzibar jinsi ya kutunza ,mapato yao ya biashara ya saloon katika uwanja wa Amaan leo jioni saa 10.30.

Kwa mujibu wa Mratibu wa mchezo huo unaotarajiwa kufanyika leo,amesema timu yake ya PBZ imejiandaa vya kutosha katika mchezo huo na kutowa kipigo cha magoli yasiozidi 4, kwa timu hiyo ya salon, na kuonesha jinsi wanavyocheza soka na kutowa kipigo kwa nduzu zao wa BOT, wiki iliopita cha mabao 2--0.

Nao vijana wa salon wamesema watatowa fundisho kwa timu ya PBZ jinsi ya kusakata mchezo huo na kutowa kipigo kisichozidi mabao 5-0 waende kutowa huduma kwa wateja wao wakiwa na machovu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.