Habari za Punde

Mafunzo ya Wajasiriamali Kazi NjeNje.

Miza Othman-Maelezo Zanzibar Imeelezwa kuwa iwapo Wahitimu waliopata Mafunzo ya Ujasiriamali watakuwa na umoja na mashirikiano katika kufanya biashara zao kutawawezesha kuondokana na umasikini wa kipato.

Haho yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Kazi na Ajira, Ameiri Ali Ameiri alipokuwa akifunga mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika katika Skuli ya Msingi Magogoni Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Wananchi wengi wamekuwa wakipata mafunzo ya Ujasiriamali lakini kinachokosekana ni ushirikiano mdogo miongoni mwao jambo ambalo huwarudhisha nyuma kimaendeleo.

Ameongeza kuwa kupata elimu ya Ujasiriamali humuezesha mwananchi kujua namna bora ya kuyakabili maisha kupitia elimu aliyopata na kujikomboa na umasikini.


‘’Nakuombeni sana Elimu mliyopata ya ujasiriamali muitumie vizuri na mushirikiane vya kutosha katika kufanya biashara zenu ili mabailiko yaonekane kwa haraka hapa Magogoni” Alisema Ameiri Ali Ameiri.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Ujasiriamali kutoka Kazi nje nje Abubakari Hussein Talib amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwawezesha Wajasiriamali kubuni Miradi tofauti ya kibiashara ili kujiletea maendeleo katika shehia yao na maisha yao kwa ujumla.

Aliwataka Wahitimu hao kubuni mawazo mapya ya kibiashara ambayo yatawafanya kujiongezea kipato na kubadili maisha yao kulingana na Mitaji yao.

‘’Kubuni wazo zuri la kibiashara ni kuleta maendeleo na kuipamba biashara ni kupata wateja waliobora katika biashara yako’’. Alisema Abubakari Hussein.

Diwani wa Shehia ya Magogoni Moh’d Suleiman Rajabu amesema Wananchi wanapaswa kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali yatakayowawezesha kujiajiri wenyewe ili kuepukana na dhana ya kuitegemea Serikalini katika ajira.

Mafunzo hayo ya Ujasiriamali kwa wananchi hao yamefadhiliwa na Mbunge wa jimbo la Magogoni Hamad Ali Hamad kwa kushirikiana na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa lengo la kuwakomboa wananchi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.