jamhuri ya muungano wa tanzania
WIZARA YA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MKUTANO WA
26 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Mkutano
wa 26 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki umekwisha
leo jijini Arusha. Mkutano huo ambao ulianza kwa ngazi ya Wataalam tarehe 22-23
Aprili, 2013 na kufuatiwa na wa Makatibu Wakuu tarehe 24 Aprili, 2013 umepokea
taarifa ya hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inatarajiwa kutiwa saini na Wakuu wa Nchi
Wanachama katika Mkutano wao wa 15, mwezi Novemba, 2013.
Aidha,
Mkutano ulijadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa Mamlaka ya Mahakama ya
Afrika Mashariki.
Vilevile,
Baraza la Mawaziri limepokea na kujadili mapendekezo ya bajeti ya Jumuiya kwa
mwaka 2013/14 na limeridhia mapendekezo ya bajeti ya Jumuiya kwa mwaka 2013/14
kuwa Dola za Marekani 117,238,966.
Mkutano
huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa
Itifaki ya Hadhi na Kinga kwa
watumishi wa Jumuiya na Taasisi zake.
Imetolewa
na
KATIBU
MKUU
WIZARA
YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
No comments:
Post a Comment