Na Mwandishi maalum
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amemteua, Hamad Bakari Mshindo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar.
Dk. Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa katika kifungu cha 11(1)(a) cha Sheria namba 11 ya mwaka 2008 iliyounda Shirika hilo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi wa Mshindo umeanza Aprili 24 mwaka huu.
Kwa kweli Mshindo ni hazina ambayo SMZ imeshindwa kuitumia ipasavyo!
ReplyDeleteUwezo wa kielimu na kiakili alionao Mshindo huwezi kumfananaisha na viongozi wengi wa SMZ!
Pia kama kuna viongozi watatu tu wa SMZ wanaoipenda CCM basi Mshindo anaweza akawa mmoja wao tena sio wale maslahi bali wale wa ukweli!..lkn. wapi!!!