Habari za Punde

PBZ Yaendeleza Ubabe kwa timu pinzani Zanzibar

Kikosi  kazi cha timu ya PBZ, kikiwa katika picha ya pamoja, kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kujipima nguvu, ambacho hutowa kichapo kwa wapinzani wao wanaocheza na.timu hii ikiwa katika mazoezi yake makali ya kujiandaa na Ligi ya Mabenki inayotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi wa Juni, katika uwanja wa Mao Unguja.  
 Nahodha wa timu ya PBZ akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza cha mchezo, wao wa kukiendelea na kukipa mazoezi ya kujiandaa na michuano ya mabenki.
  Kikosi cha Timu ya Mtakimwu  ilioilazimisha timu ya PBZ kutoka nao sare ya mabao 1--1, katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Afya Mbweni, wakiwa na Meneja wao na Mktakimwu Mkuu. Mohammed Hafidh, katikati.  

 Beki wa timu ya PBZ  Ussi Nahoda, akizuiya mpira katika mchezo wao wa kujipima nguvu na timu ya Mtakimwi, uliofanyika uwanja waChuo cha Afya Mbweni.timu hizo zimetoka sare ya mabao 1-1  
 Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Mktakimwi Yussuf Mansoor, akiwapita wachezaji wa timu ya PBZ, katika mchezo wa timu hiyo ikiwa katika maandalizi ya Ligi ya Mabenki Zanzibar, inayotarajiwa kufanyika mwezi wa juni na kushirikisha timu zote za mabenki yalioko Zanzibar.   
 Mtakimwi Mkuu wa Serekali Zanzibar Mohammed Hafidh,(mwenye fulana ya mistari) akifuatilia timu yake ilipokuwa ikicheza na timu ya PBZ katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika uwanja wa Afya Mbweni Unguja.
 Viongozi wa timu yaPBZ wakifuatilia mchezo wa kujipima na timu ya Mtakimwi Mkuu wa Serekali, uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Afya Mbweni. timu hizo zimetoka sare 1--1

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.