Wananchi wa Kihinani na Kihinani matopeni wamepata faraja baada ya kujengwa daraja katika mto ambao hujaa maji na kupita kwa kasi na kuhatarisha Watoto na wananchi wanaotumia njia hiyo kuwafikisha majumbani kwao.
Daraja hililimeleta afueni kwa Wananchi wanaotumia njia hii kwa kuweza kuvuka kwa usalama na watoto wao wanaporudi skuli hupita bila ya mashaka na kuhofia usalama wao wakati wa mvua na kujaa kwa mto huo unaopitisha maji yanayotoka kihinani juu na kupelekwa katika bonde la mpunga la chuini.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema daraja hili limekuwa mkombozi wao wakati wa mvua huwa na wasiwasi na watoto wao wanapokuwa wakirudi skuli.
No comments:
Post a Comment