Waziri Mkuu wa Serikali Ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akitoa shukrani baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 50,000,000/- iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya wananchi waliopatwa na maafa kufuatia kunaguka kwa jingo la ghorofa 16 kati kati ya Jiji la Dar es salaam hivi karibuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 50,000,000/- iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kuwafariji wananachi waliofikwa na maafa kufutia kuanguka kwa jnego la ghorofa 16 Jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Osterbay Jijini Dar es salaam.
Picha na Hassan Issa wa - OMPR – ZNZ
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa mkono wa Pole kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia ajali ya Jengo la Ghorofa 16 lililoanguka hivi karibuni Katika Mtaa wa Indira Ghandi Mjini Dar es salaam na kusababisha maafa makubwa yaliyopelekea vifo vya watu wasiopunguwa 36.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitowa mkono huo wa pole kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati akikabidhi Hundi ya shilingi milioni 50,000,000/- kwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Piter Pinda.
Makabidhiano hayo yamefanyika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyopo Mtaa wa Osterbay Jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Serikali zote mbili.
Balozi Seif alisema maafa yaliyowapata wananchi hao ambapo wengine wamefariki dunia na baadhi kujeruhiwa yameugusa umma wote wa Watanzania Bara na Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwataka wananchi waliopatwa na maafa hayo ambao wengine tayari wameshapata vilema vya maisha kuwa na moyo wa subra na kuelewa kuwa hiyo ni miongoni mwa mitihani ya mwenyezi Muungu.
Alisema katika kuungana na wananachi hao katika msiba na maafa hayo serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewaombea duwa wale walioko Hospitalini wapone haraka ili waungane na ndugu na jamaa zao katika harakati zao za kimaisha za kila siku.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar katika msafara huo amefuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibae Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Wengine aliofuatana nayo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni katibu wa Kamati ya Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohd pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar Nd. Khamis Mussa.
Akipokea Hundi hiyo Waziri Mkuu wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Piter Pinda ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa juhudi na moyo wake iliyouonyesha wa kuujngana na wenzao wa Bara kutokana na Maafa hayo.
Mh. Pinda alisema juhudi hizo zimeonyesha namna ya Viongozi na wananchi wa pande zote mbili za muungano wanavyoshirikiana katika raha na matatizo na kusaidiana na kuyatatua pale inapobidi.
“ Kitendo hichi cha SMZ cha kukubali kuungana na wenzao wa Bara kinadhihirisha ule usemi wa wahenga unaoelezea kuwa akufaae kwa dhiki ndie rafiki”. Alifafanua Waziri Mkuu wa SMT Mh. Pinda.
Zoezi la uokozi wa watu waliofunikwa katika Jengo hilo la ghorofa 16 lililoporomoka likiwa katika harakati za ujenzi lilisimamishwa rasmi tarehe mosi April mwaka huu.
No comments:
Post a Comment