Habari za Punde

Wahabeshi 63 Mbaroni

Na Kija Elias, Moshi
WAHAMIAJI haramu 63 raia wa Ethiopia wanashikiliwa na polisi mkoani Kilimanjaro kwa kuingia nchini kinyume cha sheria.

Kaimu Kamanda Polisi mkoani hapa, Koka Moitika amethibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao ambapo,alisema wamekamatwa katika matukio mawili tofauti.

Alisema wahamiaji hao walikamatwa Aprili 10 na 11 mwaka huu katika nyakati tofauti katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.


Moita alisema tukio la kwanza lilitokea Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 06:45 katika eneo la Mikocheni Kituri wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, ambapo askari hao wakiwa katika dori waliwakamata raia hao wakiwa wamejificha katika vichaka.

Alisema askari hao wakiwa doria waliwakamata raia 53 na kuwapeleka katika kituo kikuu cha polisi mjini Moshi kwa mahojiano zaidi.

Alisema katika tukio la pili ambalo lilitokea Aprili 11 mwaka huu majira ya saa sita usiku eneo la Mlaki B Kileo tarafa ya Mwanga mkoani humo, askri hao wakiwa katika doria waliwakuta wahamiaji haramu 10 raia wa Ethiopia wakiranda randa huku wakiwa hawajui mahali pa kwenda, ndipo askri hao waliwatilia shaka na kuwakamata kwa ya mahojiano zaidi.

Alisema wahamiaji hao wako katika kituo kikuu cha poisi mjini Moshi kwa mahojiano zaidi ili jeshi hilo lieendele na uchunguzi wa kuwatambua watu wanaowasaidia kuwasafirisha ili sheria ziweze kuchukua nafasi yake.

Alitoa wito kwa wanachi kuendelea kushirikiana na polisi ili kuwabaini wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia nchi kinyume cha sheria.

Wakati wahamiaji haramu hao wakikamatwa mkoani hapa tayari maofisa wa uhamiaji nchini wapo mkoani Kilimanjaro kwa semina ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili idara hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.