Habari za Punde

Abiria wa Anga Wafikia Milioni 4


Na Joseph Ngilisho Arusha
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga nchini, imefanikiwa kuongeza idadi ya abiri kutoka milioni 2.1 mwaka 2005 hadi milioni 4.1 mwaka 2012, ikiwa ni ongezeko la asilimia 90.

Aidha abiria katika viwanja vya Kilimanjaro na Arusha, wameongezeka kutoka 360,331 hadi 715,356 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 98.5.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Fadhil Manongi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la mamlaka ya Usafiri wa Anga, unaofanyika jijini Arusha.

Alisema ongezeko jingine wanalojivunia ni kuongezeka kwa mashirika ya ndege ya kimataifa kutoka 12 mwaka 2005 hadi 17 2013.


“Hali hii imetuwezesha kuongeza safari za kimataifa kwa wiki kutoka 87 hadi 209 katika kipindi hicho na hili ni ongezeko la asilimia 134.8,” alisema.

Manongi alisema mafanikio hayo yametokana na jitihada za serikali kuumarisha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro, hali iliyochangia mashirika mengi ya kimataifa kuweza kufanya safari zake.

Adha alisema juhudi hizo zimeleta mafanikio makubwa, kwani mashirika ya ndege ya Uturuki, Kenya (KQ) na Qatar Airways yameanza kufanya safari katika uwanja huo kwa siku za karibuni.

Pia mashirika yaliopo yameongeza idadi ya safari kuingia na kutoka uwanjani hapo, ambayo ni Ethiopia, Uganda Airlines na RwandaAir.

Pamoja na mafanikio hayo, amekiri kuwa bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutoweza kuleta ndege za mizigo za kubeba maua na bidhaa nyengine za kilimo zinazotakiwa kwenye masoko ya Ulaya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.